Mamia ya wakazi wa Kibiko, Kaunti ya Kajiado, waliandamana na kufunga barabara nje ya mahakama ya Ngong wakipinga kukamatwa kwa watu wawili kufuatia mzozo unaoendelea wa ardhi.
Wawili hao walifikishwa mahakamani ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya kuchoma gari na kusababisha taharuki wakati wa makabiliano kati ya makundi mawili yanayodai umiliki wa ardhi ya Kibiko. Waandamanaji walidai kuwa wenzao wamekamatwa kimakosa huku wakiitaka serikali kuingilia kati ili kuhakikisha haki inatendeka.
Mgogoro wa umiliki wa ardhi ya ekari 2,600 ya jamii ya Keekonyokie umedumu kwa zaidi ya miaka kumi, na umekuwa chanzo cha mizozo ya mara kwa mara. Kesi hiyo iliendeshwa kwa njia ya mtandaoni, ambapo washukiwa waliachiliwa kwa dhamana...