Kwenye ziara yake katika afisi za usajili hapa jijini Nairobi ambako mashine mpya zenye uwezo wa kuchapisha vitambulisho 16,000 kwa siku zilizinduliwa, Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen alisema kuwa zaidi ya vitambulisho 400,000 vitapelekwa kwa machifu wa maeneo mbalimbali ili wasaidie kuzisambaza kwa wananchi na kutoa suluhu kwa mrundiko wa vitambulisho ambavyo havijachukuliwa.Murkomen pia alisisitiza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha uwazi kwenye utoaji wa huduma kwa umma. Wanaosajiliw akuchukua vitambulisho kwa mara ya kwanza hawahitajiki kulipa chochote.