Milipuko na mizinga yaitikisa Gaza, Israel kuendeleza vita Rafah

  • | VOA Swahili
    542 views
    Milipuko mikubwa ya mabomu inayotokana na mashambulizi ya anga na mizinga iliyorushwa iliutikisa upande wa kaskazini mwa Gaza Jumamosi (Mei 11), moshi uliokuwa ukitoka katika majengo ulionekana kutoka Israel huku mapigano kati ya Israel na Hamas yakiendelea. Jeshi la Israel lilisema limewataka wakaazi na watu wasiokuwa na makazi katika eneo la Jabalia la kaskazini mwa Gaza kuondoka, linasema linarejea operesheni yake huko baada ya kutambua Hamas wanajaribu kujiimarisha ili walidhibiti eneo hilo. Israel pia ilisema imewataka Wapalestina katika maeneo mengine kusini mwa Gaza katika mji wa Rafah kuondoka na kuelekea kwa kile walichokiita eneo lililopanuliwa la kibinadamu huko Al-Mawasi, ikiwa ni ishara kwamba jeshi hilo linashinikiza kuendelea na mipango yake ya mashambulizi ya ardhini huko Rafah. Wizara ya Afya ya Palestina ilisema Wapalestina wasiopungua 37, 24 kati yao ni kutoka eneo la kati la Gaza, waliuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika usiku kucha katika eneo hilo finyu, ikiwemo Rafah, mji wa upande wa kusini zaidi wa Ukanda huo unaopakana na Misri. Haitofautishi ni watu wangapi kati yao ni raia au wanamgambo. Jeshi la Israeli lilisema ndege yake ilipiga malengo kumi eneo la Gaza katika siku iliyopita, ikiongeza majeshi yake ya ardhini yalikuwa yametokomeza wapiganaji takriban 30 huko Zeitoun. Vita kati ya Israel na Hamas vilianza baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.⁣ - Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #helikopta #shambulizi #unrwa #un