Viongozi wa ODM Kaunti ya Lamu, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Aisha Nizar, wamepongeza muungano wa Chama cha ODM na Serikali ya Kenya Kwanza, wakisema umeleta maendeleo makubwa katika kaunti ya Lamu.
Kadhalika, wanasema kuwa uhusiano huo umesaidia kuimarisha sekta ya usalama ambayo awali ilikabiliwa na changamoto nyingi. Wakizungumza katika Sherehe ya maadhimisho ya Miaka Ishirini ya chama hicho, viongozi hao wametoa wito Kwa IEBC kufanya uhamasisho Wa usajili wa Kura Mashinani huku wakiwataka vijana kujitokeza Kwa wingi kujisajili ili wapate usemi kwenye debe.