Wetangula awataka wabunge kutowapotosha wananchi kuhusu mswada wa fedha wa mwaka wa 2024

  • | Citizen TV
    287 views

    Spika wa bunge la Kitaifa Moses wetang'ula amewarai kuacha kujadili mswada wa fedha wa mwaka 2024/25 kwenye mikutano ya hadhara ilhali wana majukumu ya kutunga sheria na kurekebisha masuala ambayo hawakubaliani nayo. Akizungumza katika hafla ya mazishi ya Mzee Yonah Namuli Katika Kijiji Cha Sanandiki eneo Bunge la Kabuchai, Wetang'ula amesema kuwa kuna baadhi ya wabunge ambao wameanza kupinga Mswada huo wa Fedha ilhali wananchi bado wanatoa maoni yao na bado nafasi ya kuujadili bungeni haijafika.