- 310 viewsDuration: 1:49Wanafunzi wa chuo kikuu cha Moi wameandamana jijini eldoret kulalamikia mgomo wa wahadhiri unaoendelea kwa wiki ya nne sasa. Wanafunzi hao wanasema wamelipa karo na hawataendelea kuvumilia na kupoteza muda wao chuoni ilihali wanagharamikia hasara ya chakula na kodi ya nyumba. Wanaitaka wizara ya elimu kusuluhisha mzozo wa mkataba wa makubaliano ambao wahadhiri wanasema wanaidai serikali shilingi bilioni 7.9.