Hezbollah yasema imeshambulia kituo cha jeshi la Israel

  • | VOA Swahili
    1,229 views
    Moshi ulikuwa umesambaa katika eneo la mpakani la kaskazini mwa Israel Alhamisi (Mei 16) baada ya msururu wa makombora kufyatuliwa kutoka Lebanon na kupiga maeneo ambayo hayana watu, huku Hezbollah ikiwa inafanya mashambulizi kwa kutumia droni na makombora yanayopigwa bila ya shabaha. Taarifa ya Jeshi la Israeli iliyochapishwa saa kadhaa baada ya ving’ora kusikika katika jamii za Israeli zinazopakana na Lebanon, ilisema zaidi ya makombora 40 yalionekana yakivuka mpaka kutoka Lebanon, baadhi yake yalitunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya jeshi la Israeli na hakuna yaliyosababisha majeruhi. Siku ya Jumatano (Mei 15), Hezbollah ilisema imefanya shambulizi la droni katika kituo cha kijeshi magharibi mwa Israel huko Tiberias ikiwa ni shambulizi la ndani zaidi katika eneo la Israeli tangu kikundi chenye silaha cha Lebanon kilipopambana na Israel sambamba na vita vya Gaza. - Reuters #hezbollah #wapiganaji #lebanon #Israel #tiberias #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #helikopta #shambulizi #unrwa #un