Tanzania kuendelea kuiunga mkono sera ya China-moja

  • | VOA Swahili
    709 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Yusuf Makamba mjini Beijing Ijumaa. Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Kitengo cha Siasa cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, alimkaribisha Makamba kwa ziara yake nchini China katika maadhimisho ya miaka sitini tangu kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Wang alisema urafiki kati ya China na Tanzania una msingi imara na unatoa mfano mzuri juu ya mshikamano kwa nchi zinazoendelea na ushirikiano wa pamoja. Wang alisema kuwa China inathamini uungaji mkono wa muda mrefu kwa Tanzanai katika masuala muhimu yanayohusu maslahi ya China, na iko tayari kuendelea kuimarisha kuiunga mkono Tanzania katika kulinda uhuru, usalama na maslahi ya kimaendeleo. China inaiunga mkono Tanzania kwa uamuzi wake wa kutafuta njia ya maendeleo ambayo inakidhi haki yake ya kitaifa na kupinga uingiliaji kati wa mataifa ya nje, alisema Wang. China iko tayari kuendeleza uaminifu wa kisiasa wa pande mbili, kujenga misimamo ya kimkakati na kupanua ushirikiano na Tanzania, Wang alisema. Kwa upande wake, Makamba alisema kuwa Tanzania na China zinaendelea kufurahia utamaduni wa kirafiki. Tangu kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikiaminiana na kusaidiana. . Tanzania itaendelea kusimama imara kuunga mkono sera ya China-moja na kutotetereka kuiunga mkono China katika masuala yanayohusu maslahi muhimu ya China na kero kubwa mbalimbali. Tanzania inaridhia kabisa na kuunga mkono kikamilifu nadharia ya kujenga umoja wa kijamii kwa kuwa na lengo la mustakbali wa pamoja wa kibinadamu, na juhudi za Belt and Road Initiative na juhudi tatu kubwa za kimataifa, ambazo zilipendekezwa na Rais Xi Jinping, Makamba alisema. Wakati wa mkutano wao, mawaziri hao pia walijadili pia mkutano mpya wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika ambao utafanyika kipindi cha majira ya vuli huko Beijing na kueleza azma yao ya kutoa michango mikubwa zaidi kulinda maslahi ya pamoja ya ukanda wa Kusini wa Dunia. #tanzania #china #chinamoja #sera #ukomunisti #ujamaa #voa #voaswahili