Majira ya asubuhi Jumapili (Mei 19) kikundi cha watu takriban 50 waliokuwa na silaha walishambulia makazi ya waziri mkuu, waziri wa ulinzi na mwanasiasa mwingine mwandamizi, kulingana na jeshi.
Walivunja sheria pia kwa kuingia katika Kasri ya Taifa ambayo ni ofisi ya Rais Felix Tshisekedi.
Kanda za video katika mitandao zilwaionyesha washambuliaji wakipandisha bendera ya Zaire, jina la zamani la Congo.
Mara baada ya hapo, vikosi vya usalama viliingia ndani.
Kiongozi wa kikundi hicho, mwanasiasa wa Congo aliyekuwa anayishi Marekani Christian Malanga, na wengine watatu waliuawa.
Watu wengine 40 walikamatwa, jeshi lilieleza.
Christian Malanga ni nani?
Malanga alijiita kuwa ni “Rais wa Zaire Mpya” na mkuu wa serikali iliyo uhamishoni katika tovuti yake.
Tovuti haikueleza mipango ya kukamata madaraka kwa nguvu.
Kulingana na wasifu wake uliopo katika mtandao, mtu huyo mwenye umri wa miaka 41 alihamia Marekani kama mkimbizi mtoto.
Alirejea Congo kutumikia kama afisa wa jeshi aliyepambana na waasi huko mashariki, ilisema taarifa, na alifanya kampeni dhidi ya wanasiasa walioko madarakani hivi sasa ambao aliwashutumu kwa rushwa na utawala mbaya.
Kulingana na msemaji wa jeshi Sylvain Ekenge, Malanga jaribio la kwanza la mapinduzi lilikuwa mwaka 2017.
Nani waliohusika ?
Ekenge alisema raia watatu wa Marekani, akiwemo mtoto wa Malanga, ni kati ya wale waliokamatwa.
“Hawa raia wa kigeni na raia wa Congo walidhibitiwa, wakiwemo viongozi wao.”
Ekenge identified one of the assailants as U.S. citizen Benjamin Zalman-Polun.
Ekenge alimtambua mmoja wa washambuliaji kuwa ni raia wa Marekani Benjamin Zalman-Polun.
Vyombo vya habari vya eneo vilimuelezea mtu huyo kuwa ni mfanyabiashara wa dawa za bangi ambaye pia alijihusisha na uchimbaji madini kwa kushirikiana na Malanga.
Zalman-Polun na wawakilishi wake hawakuweza kupatikana kutoa maoni.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema imesikitishwa na ripoti za raia wa Marekani kuhusika na jaribio la mapinduzi.
Hii linamaanisha nini kwa Congo?
Kasi ambayo jaribio hilo la mapinduzi lilizimwa inaonyesha waliokuwa wamepanga hawakuwa tishio kubwa.
Hata hivyo kuna wasiwasi – kama anavyoeleza mkaazi wa Kinshasa Ramazani Salabuni.
“Kinacho tushangaza ni kwamba kuna walinzi wengi wa rais katika Kasri ya Taifa, lakini watu hawa waliweza kuingia kwa urahisi na walikuwa wana silaha.”
Hilo linaleta maswali kuhusu usalama ndani ya jiji hili.
Tukio hili pia limekuja wakati nyeti sana kwa Tshisekedi.
Anafanya juhudi za kudhibiti mashambulizi ya waasi yanayoendelea kwa miaka miwili huko mashariki mwa Congo.
Miezi mitano baada ya kutokea upinzani juu ya kuchaguliwa tena, muungano wa utawala wa Tshisekedi umeshindwa kuunda serikali kutokana na mivutano ya ndani kuhusu nafasi za kazi – licha ya kuwa ni wengi ndani ya Bunge.
Mwisho…