- 17,733 viewsDuration: 1:16Viongozi wa chama cha ODM wamewashutumu vikali viongozi wa upinzani kufuatia matamshi yao hapo jana kuhusu afya ya kinara wa chama hicho Raila Odinga. Viongozi hao wakiwemo manaibu vinara wa ODM Abdulswamad Sharrif Nassir, Godfrey Osotsi na katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna, wamewataka viongozi hao kukoma kumkejeli Odinga kwa kutumia hali yake ya afya.