Wanaume kaunti ya Migori kupigania maslahi ya mtoto msichana

  • | Citizen TV
    254 views

    Wakereketwa wanaopigania maslahi ya mtoto msichana wameanza kuwahusisha wanaume kwenye mikakati ya kukabiliana na ndoa za utotoni Wakizungumza baada ya kongamano la siku mbili, washikadau hao Kutoka kaunti za Migori na Homa bay walikiri kwamba Nia Yao ni kupunguza ndoa na mimba za utotoni pamoja na ukeketaji miongoni mwa watoto Kwa kiasi kikubwa. Washikadau hao wanasema kuwa kuwahusisha wanaume kutasaidia pakubwa kukabili changamoto hizo na kuepuka mienendo potovu katika jamii.