Kesi dhidi ya Paul Mackenzie yaanza kusikizwa

  • | Citizen TV
    923 views

    Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa imeanza kusikiliza kesi dhidi ya mhubiri tata Paul Mackenzie na washukiwa wenzake 94. Kesi hiyo imeanza baada ya pande zote kuafikiana jinsi itakavyosikizwa huku mashahidi zaidi ya 60 wakitarajiwa kutoa ushahidi wao. Hata hivyo wanahabari walizuiwa kufuatilia kesi hiyo ambapo shahidi wa kwanza ambaye yuko chini ya ulinzi anatoa ushahidi wake dhidi ya washukiwa hao.Katika kesi hiyo Mackenzie na wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne yanayohusiana na ugaidi. Washukiwa hao wakiwa wafuasi wa kanisa la Good News International wanadaiwa kuhusika na vifo vya watu zaidi ya 430. Kesi hiyo inaendelea mbele ya hakimu mkuu Leah Juma.