Madaktari waandamana kushinikiza wanafunzi waajiriwe

  • | Citizen TV
    2,900 views

    Madaktari wameandamana hadi katika wizara ya afya kushinikiza kuajiriwa kwa madaktari wanagenzi. madaktari hao wanailaumu wizara ya afya kwa kukiuka makubaliano yaliyoafikiwa na ambayo yalisababisha kusitisha mgomo wa siku 56. katibu mkuu wa KMPDU Davji Atellah amesema kuwa madaktari na wizara ya afya wamekuwa wakifanya mikutano iliyoliafikia kuwa madaktari wanagenzi wangeajiriwa katika siku 60 kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano. makataa ya siku 60 yalikamilika hapo jana.