Wanachama wa ODM eneo la Magarini wataka uteuzi wa wagombea

  • | Citizen TV
    364 views

    Baadhi ya wanachama wa chama cha ODM katika eneo bunge la Magarini, Kaunti ya Kilifi, wanataka chama hicho kufanya mchujo kabla ya uchaguzi mdogo unaokaribia.Wanachama hao wanawataka vigogo wa ODM kuwapa nafasi kumchagua mgombea wao badala ya chama hicho kuteua mgombea moja kwa moja. wanachama wawili wa chama cha chungwa wameonyesha nia ya kuwania kiti hicho. uchaguzi wa Harrison Garama Kombe ulibatilishwa na mahakama.