Shambulizi la Israel laua 23 na kujeruhi wengine katika shule ya UNRWA

  • | VOA Swahili
    119 views
    Shambulizi la anga la Israeli katika shule inayoendeshwa na UN ambayo inazihifadhi familia katika kambi ya Nuseirat imewauwa watu 23 na kuwajeruhi wengine wengi, maafisa wa afya wa Palestina walisema Jumanne (Julai 16). Jeshi la Israeli lilisema katika taarifa yake limeshambulia kikundi cha “magaidi” ambao walikuwa wanafanya operesheni zao ndani ya shirika la Umoja wa Mataifa la Ujenzi na Misaada (UNRWA), baada ya kuchukua hatua za kuwaondoa raia waliokuwa hatarini katika eneo hilo. “Muda mfupi uliopita, kwa kutumia taarifa za kijasusi zilizo sahihi za Jeshi la Ardhini la Israeli na Shirika la Usalama la Israeli, Jeshi la Anga la Israeli IAF liliwashambulia magaidi waliokuwa wanafanya operesheni zao katika shule ya UNRWA katika eneo hilo la Nuseirat,” taarifa ilisema. Iliongeza kuwa IDF inafuatilia ripoti ya kuwa raia kadhaa walijeruhiwa kutokana na shambulizi hilo. Vita hiyo ilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji kutoka Palestina wa kikundi cha wanamgambo wa Hamas walipovamia mpakani na kushambulia jamii mbalimbali huko Israel, ikiuwa watu 1,200 na kuwateka watu 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israeli.⁣⁣⁣ Shambulizi la Israeli huko Gaza kulipiza kisasi lilianza siku hiyo hiyo kwa kushambulia kwa mabomu na limeendelea kwa miezi tisa pamoja na uvamizi wa ardhini ambapo mamlaka za afya Palestina zinasema imeuwa zaidi ya watu 38,000 na kujeruhi zaidi ya watu 80,000.⁣⁣⁣ Idadi kubwa ya waliojeruhiwa kutokana na vita hivyo imeongeza magonjwa kusambaa na utapiamlo kati ya wakazi asilimia 90 wa Gaza ambapo Umoja wa Mataifa unasema wamekoseshwa makazi, na kuweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya katika eneo hilo finyu.⁣ - Reuters⁣⁣ ⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #hospitali #nasserhospital