Meya wa Paris aogelea mto Seine kuthibitisha unafaa kutumika kwa Olimpiki

  • | VOA Swahili
    69 views
    Meya wa Paris, Anne Hidalgo, aliogelea katika maji yenye matope ya Seine Jumatano kuonyesha kuwa mto huo hivi sasa ni msafi kabisa kwa ajili ya matukio ya kuogelea wakati wa michezo ya Olimpiki. Akiwa amevaa miwani maalum ya kuogelea na nguo za kuogelea, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 aliogelea kifudifudi kabla ya kuuzamisha uso wake na kutambaa ndani ya maji, akikamilisha takriban mita 100 kwenda na kurudi katika mto huo. Alikuwa ameogelea akiwa na maafisa wa ngazi ya juu na Tony Estanguet, mshindi wa medali ya dhahabu mara tatu katika mashindano ya kuendesha mtumbwi, anayeongoza kamati ya maandalizi ya Michezo ya Paris, itakayo funguliwa wiki ijayo Julai 26. “Leo ni uthibitisho kuwa tuko pale ambako tulitarajia kuwa,” Estanguet alisema. “Hivi sasa tuko tayari kuandaa michezo hiyo huko Seine.” Licha ya uwekezaji wa euro bilioni 1.4 ($1.5 bilioni) kuzuia maji taka kuvuja na kuingia katika mto huo, wasiwasi kuhusu mto huo umeenea katika jimbo la Seine kuelekea Michezo ya Paris. Lakini kuanzia mwezi Julai, kutokana na mvua kubwa hatimaye kumekuwa na hali ya hewa ya joto, sampuli zikionyesha mto huo uko tayari kwa ajili ya uogeleaji na mashindano ya Olimpiki. #meya #paris #olimpiki #mto #annehidalgo #voa #michezo #kuogelea #ufaransa #voaswahili