Trump akubali uteuzi wa Chama cha Republikan, siku kadhaa baada ya jaribio la kuuwawa

  • | VOA Swahili
    366 views
    Donald Trump, akikaidi na akiuguza jeraha, amefikisha ujumbe “wa kujiamini, nguvu na matumaini” katika Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Chama cha Republikan Alhamisi wakati akikubali uteuzi wa urais uliofanywa na chama chake katika hotuba ya kuwaunganisha wanachama wa Chama cha Republikan GOP – na taifa – siku tano tu baada ya kunusurika na jaribio la kuuwawa ambalo lingeweza kumaliza uhai wake. (AP) #donaldtrump #biden #uselections #PresidentialElection2024 #voa