Mwandishi alipigwa risasi mara tatu wakati akiripoti maandamano dhidi ya serikali #short #shorts

  • | VOA Swahili
    137 views
    Mwandishi wa habari Catherine Wanjeri alipigwa risasi mara tatu katika paja wakati akiripoti kuhusu maandamano dhidi ya serikali Julai 16 huko Kaunti ya Nakuru, Kenya. Wanjeri, ambaye hivi sasa anauguza majeraha yake baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa risasi anaelezea kilichotokea siku hiyo. Waandishi wa habari 13 nchini Kenya walijeruhiwa au kukamatwa wakati wakiripoti kuhusu maandamano hayo yaliyofanyika hivi karibuni dhidi ya serikali. #kenya #ruto #voaswahili