Viongozi wa kaunti ya Kwale wapinga mpango wa kulipisha utumizi wa barabara ya Dongo Kundu

  • | K24 Video
    36 views

    Viongozi wa kaunti ya Kwale wakiongozwa na Gavana Fatuma Achani wamepinga vikali mpango wa kulipisha utumizi wa barabara ya Pembeni ya Dongo Kundu. Pingamizi hiyo imeibuka siku chache baada ya madereva kuanza kutumia barabara hiyo inayounganisha kaunti za Mombasa na Kwale, na tayari wanasema imeimarisha maisha yao kwa kuokoa muda kwa kiasi kikubwa.