Serikali ya afya yasema kuwa Kenya iko salama dhidi ya maambukizi ya homa ya nyani.

  • | K24 Video
    95 views

    Serikali kupitia wizara ya afya imesema kuwa Kenya iko salama dhidi ya maambukizi ya homa ya nyani. Visa vitano vipya vinavyoshukiwa kuugua ugonjwa wa Mpox vimegunduliwa nchini, na vinasubiri uthibitisho kutoka kwa maabara. Wizara ya afya imewaonya wakenya kuhusu ucheleweshaji unaoweza kutokea katika maeneo ya kuingia nchini, kutokana na kuongezeka kwa utekelezaji wa hatua za afya za umma, kama vile uchunguzi.