Bunge la seneti lajadili hoja ya kumuondoa gavana wa Meru Kawira Mwangaza

  • | Citizen TV
    830 views

    Mawakili wa gavana wa meru kawira mwangaza wamekanusha madai dhidi ya mteja wao yaliowasilishwa na bunge la kaunti hiyo kama vigezo vya kumtimua mamlakani. bunge la seneti linaendelea na kikao cha kujadili hoja ya kumtimua gavana wa meru kawira mwangaza. wawakilishi wadi 49 walipiga kura ya kumundoa mwangaza mamlakani huku 17 wakipinga hoja hiyo. kwa mujibu wa naibu kiongozi wa wengi wa bunge hilo aliyewasilisha hoja hiyo Zipporah Kinya, mwangaza anatuhumiwa kwa kukiuka katiba, na kutumia vibaya ofisi yake miongoni mwa masuala mengine. Ikumbukwe kwamba, hii ni mara ya tatu kwa bunge la meru kumtimua gavana mwangaza. Mwangaza atajitetea kabla ya maseneta waliochaguliwa kutoa uamuzi wao kwa kupiga kura