Familia ya Lillian Gati yaomba msaada kupata mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepotea

  • | KBC Video
    297 views

    Familia moja katika eneo la Isebania huko Kuria, kaunti ya Migori inakabiliwa na hali ya wasiwasi baada ya mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 20 kutoweka . Lilian Gati Robi, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Mount Kenya, anasemekana kusafiri kwenda Nairobi jumanne usiku akielekea Thika, ambako anaendelea na masomo yake . Hata hivyo baba yake alisema hajawasiliana na familia, hata ingawa walithibitisha kwamba basi hilo liliwasili Nairobi siku ya Jumatano asubuhi na kwamba Lilian alikuwa miongoni mwa abiria waliowasili jijini.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive