Uwezo wa serikali za kaunti kutumia bajeti kikamilifu

  • | K24 Video
    14 views

    Mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakango ameelezea wasiwasi kuhusu uwezo wa serikali za kaunti kutumia kikamilifu bajeti walizotengewa. Ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa katika mwaka wa kifedha wa 2023/24, kaunti zilitumia asilimia 57.5 tu ya bajeti zao za maendeleo, ikilinganishwa na asilimia 61 ya mwaka uliopita. Nyakango katika ripoti hiyo anahofia kuwa hali hii, italemaza maendeleo katika kaunti huku kaunti nyingi zikishindwa kutekeleza miradi muhimu.