Kenya Kwanza yajivunia kubuni nafasi zaidi za ajira miaka miwili baadaye

  • | KBC Video
    66 views

    Baada ya miaka miwili afisini, serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto inajivunia gharama nafuu ya vyakula, ikiwa ni pamoja na unga wa mahindi ambayo imepigwa jeki na utoaji mbolea ya ruzuku, kubuniwa kwa nafasi zaidi ya laki mbili za ajira kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na kuimarishwa kwa shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Marekani. Hata hivyo miradi mingi ya miundo mbinu haijakamilika huku serikali ya Kenya Kwanza ikisema manifesto yake ina mpango wa miaka mitano wa utekelezaji miradi hiyo. Uongozi wa chama cha UDA, hata hivyo umesema kesi mahakamani kuhusu baadhi ya miradi na kuondolewa kwa mswada wa fedha wa mwaka 2024, vimeathiri utekelezaji wa miradi muhimu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive