Harris, Trump waanza malumbano mwanzo kabisa wa mdahalo wao

  • | VOA Swahili
    646 views
    Makamu wa Rais wa Marekani Mdemocrat Kamala Harris na Rais wa zamani Mrepublikan Donald Trump walikuwa hawajawahi kukutana mpaka usiku wa Jumanne katika mdahalo wao wa urais, lakini mara moja walianza kulumbana katika ushindani muhimu kuelekea katika uchaguzi wa Novemba 5. Wagombea hao wawili walisalimiana kabla ya kuanza mdahalo, kila mmoja akaelekea kwenye sehemu yake jukwaani katika National Constitution Center huko Philadelphia na kuanza kulumbana. Walibishana kuhusu uchumi wa Marekani, haki ya kutoa mimba kwa wanawake wa Marekani, uhamiaji katika mpaka wa Marekani na Mexico, vita vya Israel na Hamas huko Gaza, uvamizi wa Russia nchini Ukraine, na ghasia katika Bunge la Marekani Januari 6, 2021, wakati Congress ikiidhinisha Bunge likirasmisha matokeo ya uchaguzi 2020 ambao Trump alishindwa. Akieleza kushindwa kwa Trump uchaguzi wa 2020 ambapo Rais Joe Biden alishinda, Harris alisema, “Donald Trump alifukuzwa kazi na watu milioni 81. Ana wakati mgumu kulikubali hilo. Trump hivi karibuni alisema alishindwa katika uchaguzi “kwa kura chache,” lakini katika jukwaa la mdahalo Jumanne, alisema alikuwa anafanya kejeli na kukataa kukubali uhalali wa matokeo ya uchaguzi wa 2020. #harris #trump #debate #uselections #voa