Wakimbizi 278 warejeshwa Burundi kutoka kambi ya Mulongwe, DRC

  • | VOA Swahili
    369 views
    Kambi ya wakimbizi ya Mulongwe iko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya mwaka mmoja kukiwa hakuna wakimbizi wa Burundi wanaorejea nchini kwao, siku ya Alhamisi shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) liliwarejesha wakimbizi 278 walirejeshwa Burundi kutoka kambi ya Mulongwe. Wengi ya wakimbizi waliorejeshwa waliripoti kuwa mivutano kati yao na wenyeji wa Congo ilikuwa ni sababu kuu ya uamuzi wao kurejea nyumbani, wakati wengine waligusia kusikia kuwa usalama umerejea nchini Burundi. Wakimbizi wa Burundi 278 waliorejeshwa walikuwa ni familia 70. Walivuka mpaka wa Kavimvira kati ya Congo na Burundi wakisindikizwa na maafisa wa UNHCR, Mkuu wa Tume ya Taifa kwa ajili ya Wakimbizi, Usaidizi, Hatua na Misaada. Walisisitiza kuwa masharti ya uvunaji na kukataliwa kupewa ardhi yao wanayolima na baadhi ya raia wa Congo imepelekea uamuzi wao wa kurejea nyumbani. Iwapo hawa raia wa Burundi wanarejea nyumbani, shirika la UNHCR kawaida huwapatia kila mkimbizi dola 200. Takwimu kutoka UNHCR na Tume ya Taifa kwa Wakimbizi zinaonyesha kuwa kuna zaidi ya wakimbizi 430,000 raia wa Burundi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. #burundi #drc #voa