Mama mmoja apoteza wanawe 3 kwenye moto Mukuru Kwa Reuben

  • | Citizen TV
    2,133 views

    Mama mmoja katika eneo la Mukuru Kwa Njenga, eneobunge la Embakasi South, anaomboleza vifo vya wanawe watatu walioteketea kwenye moto ulizuka usiku wa kuamkia leo. Inaarifiwa kuwa moto huo ulisababishwa na mlipuko wa gesi na kuwaacha watu 70 bila makao. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, moto huo pia uliathiri shule na kanisa eneo hilo.