Masengeli aomba mahakama msamaha asema hakukusudia kukaidi mahakama

  • | Citizen TV
    7,826 views

    Naibu Inspekta Jenerali wa polisi Gilbert Masengeli ameomba msamaha kwa mahakama kwa kukosa kuhudhuria vikao vya mahakama kuelezea waliko watu watatu waliodaiwa kutekwa nyara na polisi katika eneo la Kitengela. Masengeli ameapa kuwa atahudhuria vikao vya mahakama na kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha sheria inafuatwa. Aidha ameelezea kuwa hakufanya kusudi kukataa kufika mahakamani bali alikuwa na majukumu ya kikazi yaliyomfanya kukosa kufika mahakamani. Aidha amesema kuwa anaheshimu mahakama na atawajibika. Haya yanajiri huku akikata rufaa kuhusu hukumu ya miezi sita aliyopewa na jaji Lawrence Mugambi.