Waziri wa kilimo pamoja na wanachama wa bodi watazamiwa kufika mbele ya kamati ya bunge

  • | Citizen TV
    404 views

    Waziri wa kilimo dkt. Andrew Karanja pamoja na wanachama wa bodi ya kudhibiti wadudu wanatazamiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kuhusu kilimo kufafanua madai kuwa zaidi ya madawa 250 ya kudhibiti wadudu nchini yanatumika licha ya kupigwa marufuku. Kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Nairobi dawa hizo zinachangia ugonjwa wa saratani.