Ruto ataka mageuzi katika Baraza la Umoja wa Mataifa

  • | Citizen TV
    935 views

    Rais William Ruto anashinikiza mageuzi katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kukabili changamoto zinazoibuka. Rais amesema kuwa mfumo wa umoja wa mataifa ulioko sasa umeshindwa kukabiliana na migogoro inayoibuka na haswa suala la mabadiliko ya tabianchi , kutokuwa na usawa na madeni. Akizungumza kwenye mkutano wa marais ulioangazia mustakabali wa mataifa wanachama, Ruto amesema kuwa mageuzi yatazuia mgogoro wa kimataifa.