Maoni mseto yaghubika hoja ya kutokuwa na imani na Gachagua

  • | KBC Video
    454 views

    Hoja ya kutokuwa na imani na utendakazi wa naibu rais Rigathi Gachagua iliyowasilishwa katika bunge la seneti na seneta Danstan Mungatana imeibua mdahalo mkali miongoni mwa wanasiasa huku baadhi wakisema hatua hiyo itaathiri shughuli za serikali. Baadhi ya wanasiasa walimkosoa naibu rais kwa madai ya kuikejeli serikali ambayo anahudumia huku viongozi wa kidini wakitoa wito wa kusitishwa kwa joto la kisiasa. Ripota wetu Joseph Wakhungu anachambua baadhi ya maoni hayo huku Wakenya wakisubiri uamuzi wa spika wa bunge la seneti kuhusu hatma ya hoja hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive