IGAD yazindua mikakati ya kudumisha amani mipakani

  • | KBC Video
    8 views

    Mikakati inayonuiwa kushughulikia changamoto zinazowaathiri watu wanaoishi katika maeneo ya mpakani katika upembe wa Afrika imeanzishwa. Mpango huo kwa jina The peaceful and Resilient Borderlands uliozinduliwa leo utashughulikia chanzo cha ukosefu wa uthabiti na vilevile kuimarisha maendeleo ya uchumi wa kijamii kwa minajili ya kudumisha amani na ufanisi. Waziri wa masuala ya kanda ya Afrika Mashariki na ustawishaji wa maeneo kame Beatrice Askul alisema Kenya inafanya juhudi za kuhakikisha jamii zinazoishi katika sehemu kame zinaishi kwa amani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive