Wabunge wataka mkataba wa Adani ukaguliwe upya

  • | KBC Video
    23 views

    Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu uwekezaji wa umma, masuala ya biashara na kawi imeagiza halmashauri ya viwanja vya ndege kusitisha mkataba baina ya serikali na kampuni ya Adani wa kuboresha uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kusubiri ripoti ya mhasibu mkuu. Ripoti ya ukaguzi ya mhasibu mkuu inatarajiwa kutolewa katika muda wa majuma mawili. Kamati hiyo inatahadharisha kwamba afisa yeyote atakayekiuka agizo hilo na kutekeleza mkataba huo atawajibishwa kibinafsi. Ripota wetu Abdiaziz Hashim ana maelezo zaidi kuhusu sakata hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive