Rais Ruto ahimiza mbinu za kisasa ka kukabili HIV

  • | Citizen TV
    342 views

    Rais William ruto amesema kuwa kenya inakaribia malengo yake ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi akisema kuwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa ukimwi vimepungua kwa asilimia 65. Akizungumza katika kikao cha umoja w amataifa huko newyork marekani, rais ruto amesema kuwa mbinu za jadi za kukabiliana na ugonjw ahuo havitasaidia kutokomeza ugonjwa huo, akitaka mataifa kuimarisha juhudi zao kwa kutumia teknolojia kuimarisha huduma za afya, kando na kuhakikisha kuwa matabaka yote katika jamii yanafikiwa na afya bora kwa gharama ya chini.