Wakazi wa Lodwar walalamikia giza

  • | Citizen TV
    41 views

    Wafanyibiashara mjini Lodwar wanalalamikia kukatizia stima Lodwar na viunga vyake kwa kipindi cha siku nne mfululizo.

    wakazi hao wanasema kuwa kampuni ya umeme kenya power haijatoa sababu zozote za kukatiza nguvu za umeme. mwenyekiti wa wafanyibishara Turkana Edward Okumu, amesema kuwa wafanyibiashara wanaotegemea stima wameshindwa kuchuma kipato chao cha kila siku,huku wengine wakikadiria hasara kutokana na ukosefu wa umeme. visa vya utovu wa usalama vimeanza kushuhudiwa Lodwar huku wakaazi wakitaka Kenya Power iwajibike.Kenya power inasema baadhi ya mitambo imeharibika na inakarabatiwa.