Changamoto za afya Bungoma

  • | Citizen TV
    152 views

    Mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa kwa kifaa maalum cha kunakili huduma za afya mashinani kwenye maeneo bunge yote Katika kaunti ya bungoma,juhudi hizo zinaonekana kukabiliwa na changamoto. Kifaa hicho maalum cha kidijitali kilinuiwa kunakili na kuhakikisha Kuna rekodi mufti za huduma za kimsingi za afya mashinani Kwa kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora zikiwemo huduma za matibabu na dawa Kwa wakati ufaao nyanjani. Hata hivyo changamoto za kifedha na udhaifu Katika mawimbi ya kusambaza habari zimelemaza juhudi hizo.