Zaidi ya nyumba 23,000 zitafaidika na mradi wa maji eneo la Ol Kalou

  • | Citizen TV
    96 views

    Zaidi ya nyumba 23,000 katika eneo la Ol-Kalou zitafaidi kufuatia kuzinduliwa kwa mradi wa maji unaogharimu shilingi milioni 19. Kisima cha Kirima kitaunganishw ana mabomba ya maji ambayo yatasafirisha maji katika vijiji mbalimbali eneo la Rurii, Plot-10, na Silanga. Gavana wa nyandarua Kiarie Badilisha amewataka wakazi kusaidia kulinda miundomsingi ya maji ili iweze kuwafaidi vilivyo. familia maskini zilikabidhiwa matangi ya kuhifadhi maji huku wakihimizwa kuweka mikakati ya kuvuna maji wakati wa msimu wa mvua