Hoja ya kumuondoa mamlakani naibu rais Rigathi Gachagua yaendelea kuibua hisia mseto

  • | K24 Video
    72 views

    Mkenya Dennis Ndereva kutoka Nyahururu sasa ameelekea mahakamani kutafuta agizo la kuzuia bunge kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani naibu rais Rigathi Gachagua. Haya yanajiri huku jaji Lawrence Mugambi akitoa agizo la kuzuia kukamatwa kwa wafanyikazi watatu wa Gachagua ambao mkuu wa mashataka ya umma aliidhinisha ombi la DCI kuwa washtakiwe pamoja na wabunge James Gakuya na Benjamin Gathiru. Mvutano wa kisheria ulioibuka katika mchakato wa kumng'atua ofisini naibu rais.