Amos Langat ashinda dhahabu ya michezo ya Afrika Mashiriki

  • | Citizen TV
    202 views

    Amos Langat amenyakuwa dhahabu kwenye mashindano ya shule za upili Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda. Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya Kipsuter iliyoko kaunti ya Bomet alinyakuwa dhahabu hiyo kwenye shindano la kuruka la High Jump. Mwelekezi wa chipukizi kwenye shirikisho la riadha nchini Barnaba Korir amesema wameweka mikakati ya kukuza michezo mengine kando na riadha ili kuwapa vijana fursa ya kuonyesha uwezo wao.