Sintofahamu ya SHA I Serikali yaagiza wagonjwa wote wahudumiwe

  • | KBC Video
    64 views

    Wizara ya afya imesema kuwa utekelezaji wa hazina ya bima ya kijamii ya afya unaendelea ipasavyo licha ya changamoto za hapa na pale kuhusiana na baadhi ya maswala. Kwenye taarifa wizara hiyo ilitaja maswala sita yanayoibua wasiwasi ambayo inayashughulikia huku ikikariri kwamba wakenya wanaweza kupata huduma za kimsingi za matibabu katika vituo vya afya vya level one hadi three. Haya yanajiri huku baraza la magavana likionya kwamba utekelezaji wa mpango huo wa afya huenda ukatatizika kutokana na ukosefu wa pesa. Baraza hilo lilikosoa wizara ya fedha kwa kutenga shilingi bilioni sita pekee za utekelezaji wa mpango huo licha ya kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni-100 kwa mpango huo wa afya. Mwanahabari wetu Timothy Kipnusu anatuarifu zaidi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive