Wafanyakazi wa BBC wakimbia milio ya risasi mpaka wa Lebanon na Israel

  • | BBC Swahili
    400 views
    Tazama wafanyakazi wa BBC wakikimbia kutafuta hifadhi baada ya milio ya risasi na makombora kusikika katika mpaka wa Lebanon na Israel TImu ya BBC ilikuwa ikipiga picha upande wa Israel katika mpaka huo karibu na eneo ambalo mapigano yameripotiwa kati ya Hezbollah na majeshi ya Israel. Baada ya kusikia silaha zikifyatuliwa na makombora kutoka mpakani, mwandishi wa Mashariki ya Kati Lucy Williamson na timu yake walikimbilia kujificha huku ving'ora vya tahadhari vikisikika. #bbcswahili #lebanon #israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw