Maonyesho ya utalii yakamilika Uhuru Gardens, jijini Nairobi

  • | Citizen TV
    371 views

    Maonyesho ya utalii ya mwaka huu katika Bustani ya Uhuru Gardens yalitamatika Ijumaa kwa mtindo baada ya AirAsia X kuzindua safari za moja kwa moja kutoka Kuala Lumpur, Malaysia, hadi Nairobi, Kenya, kwa ushirikiano na Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB). Hatua hii imepokelewa vyema na wadau wa sekta ya utalii nchini, huku Afisa Mkuu wa VIUTRAVEL, Felix Musa, akieleza kuwa idadi ya watalii kutoka bara Asia na ukanda wa Ghuba itaongezeka kwa kiasi kikubwa. Kenya inalenga kuvutia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2027.