Makao Chini ya Ardhi: Mwanaume ajenga nyumba kwenye shimo eneo la Butula, Busia

  • | Citizen TV
    6,202 views

    Mtazamaji hebu tafakari kuchimba shimo lenye kina cha futi tisa na kuligeuza kuwa nyumba yako. Ndio hatua ya kushangaza aliyochukua mwanamume mmoja katika eneobunge la Butula kaunti ya Busia. Kennnedy Onyango anaishi kwenye handaki hilo na mkewe na wanawe watatu. Ni kioja ambacho kimewashangaza wakazi wa eneo hilo ambao sasa wanahofia usalama wa familia hiyo chini ya ardhi. Jane Cherotich alitembelea familia hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.