Gachagua ajijitetea mbele ya umma dhidi ya mashtaka yanayomkumba bungeni

  • | Citizen TV
    5,726 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kufika mbele ya Bunge la Kitaifa kujitetea dhidi ya mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake katika hoja ya kumuondoa mamlakani. Hata hivyo, Naibu Rais tayari alianza kujitetea dhidi ya mashtaka hayo mbele ya umma maoni. Jana jioni, Naibu Rais alihutubia taifa na kukana madai kwamba amekiuka katiba, kufanya uhalifu, na kumdharau mkubwa wake, Rais William Ruto, huku akiishambulia serikali. Brenda Mulinya anaripoti kuhusu mahojiano ambayo yameelezewa kuwa ya kuchukiza na Spika wa Bunge la Kitaifa.