Waziri Joho asema ardhi ya Base Titanium haitarejeshewa wenyeji wa Kwale

  • | Citizen TV
    519 views

    Serikali kuu kupitia wizara ya madini imesema ardhi inayotumiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium haitarejeshewa wenyeji wakati kipindi cha kampuni kitakamokamilika mwishoni mwaka huu. Akizungumza baada kuzuru maeneo yanayochimbwa madini hayo, waziri wa madini na uchumi wa bahari Ali Hassan Joho amesema badala yake serikali itatumia ardhi hiyo kujenga miradi ya maendeleo itakayopendekezwa na wakazi kwenye kamati iliyoteuliwa kusikiza maoni yao kuhusiana na matumizi ya ardhi hiyo.