Maelfu ya wagonjwa wateseka kutokana na matatizo ya SHA

  • | Citizen TV
    390 views

    Maelfu ya wakenya bado wanatumia fedha zao kujilipia huduma za matibabu katika hopsitali za umma, licha ya serikali kutoa hakikisho la kuondoa dhiki hiyo chini ya mamlaka ya SHA. Wakenya wengi wanaishutumu serikali kwa utepetevu baadhi yao wakidai kuwa licha ya kufanya malipo zaidi ya awali chini ya bima ya afya ya NHIF, fedha hizo bado hazijahamishwa hadi SHA. Laura Otieno alitangamana na baadhi ya wagonjwa hao na kuandaa taarifa ifuatayo.