Wizara ya afya yaondoa hofu kuhusiana na usalama wa chanjo ya 'polio'

  • | Citizen TV
    260 views

    Wizara ya Afya imeondoa hofu kuhusiana na usalama wa chanjo ya polio. Naibu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Sultan Matendechero, amewahakikishia wazazi na walezi kwamba madhara yanayoripotiwa miongoni mwa watoto waliopewa chanjo ya polio ni ya kawaida na yanatarajiwa katika zoezi lolote la chanjo. Na kama anavyoripoti Mary Muoki, Naibu mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya amesema serikali imebuni timu ya wataalamu kuchunguza madai ya athari mbaya zinazoripotiwa na wazazi, huku akiongezea kuwa kufikia sasa, uchunguzi unaonyesha kuwa chanjo hio ni salama na hakuna haja ya wasiwasi au taharuki.