Hatibu Mwaura apuuzilia mbali madai kwamba nyumba za gharama nafuu zitawafaidi watu wachache

  • | KBC Video
    106 views

    Hatibu wa serikali Isaac Mwaura amepuuzilia mbali madai kwamba nyumba za gharama nafuu zitawanufaisha watu wachache pekee wenye ushawishi serikalini. Akizungumza jijini Nairobi Mwaura alisema serikali imepiga hatua kubwa kuhakikisha ufanisi wa mradi huo katika lengo lake la kubadilisha maisha ya wakenya katika sehemu mbalimbali humu nchini hasa katika mitaa ya mabanda. Mwaura alisema serikali kufikia sasa imejenga nyumba elfu 124 huku lengo likiwa kukamilisha ujenzi wa nyumba elfu 250 kabla ya mwisho wa mwaka.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive