Naibu rais aliyebanduliwa Rigathi Gachagua amzuia mteule Kithure Kindiki kuapishwa

  • | Citizen TV
    29,693 views

    Mahakama Kuu imezuia uteuzi wa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais wa tatu wa taifa hadi kesi zinazopinga kuondolewa kwa Rigathi Gachagua zitakaposikizwa wiki ijayo. Maagizo ya Mahakama Kuu yalitolewa baada ya wabunge kuidhinisha uteuzi wa Kindiki mapema Ijumaa, na Spika wa Bunge la Kitaifa kulitangaza rasmi kwenye gazeti la serikali.