Kithure Kindiki aibuka chaguo la rais Ruto kuwa naibu wake

  • | Citizen TV
    2,219 views

    Kupendekezwa kwa Abraham Kithure Kindiki na Rais William Ruto haukuwashangaza wengi kwani Minong'ono ilikuwa tayari imesambaa katika mitandao ya kijamii. Rais Ruto akionekana kurejelea uamuzi wake wa kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2022. Wakati huu akimchagua Kindiki kama Naibu Rais na Kumtema Rigathi Gachagua. Kijijini Irunduni Kaunti ya Tharaka Nithi nyumbani kwa Kindiki Shangwe na Nderemo zilitanda huku Viongozi waliomezea mate kiti hicho wakiimuunga mkono Kindiki.